Kundi la RSF limetangaza kusitisha mapigano kwa muda wa miezi mitatu hatia inayokuja ikiwa imepita siku moja baada Jeshi la sudan kukataa wito wa kimataifa wa kustisha vita unaongozwa na Marekani, kwa madai ya kuwepo kwa mapendeleo.
Kwenye hotuba iliyotolewa kupitia Televisheni Kamanda wa RSF Mohamed Hamdan Dagalo alitangaza kuwa kwa pamoja kundi hilo lilikubaliana kusitisha vita kwa muda ili kuruhusu utoaji wa misaada na kulinda raia.
Hata hivyo Dagalo aliahidi kuzingatia mfumo wa majadilino unaoshirikisha Misri, Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu, na Marekani -- pamoja na Umoja wa Afrika na mashirika mengine ya kimataifa, ili kuhakikisha na kuruhusu misaada kuwafikia raia.
Tangazo hilo la RSF limekuja baada ya mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah Al-Burhan kukataa pendekezo hilo la kusItisha vita kwa misingi ya mapendeleo kwa kundi la RSF.
RSF imeshutumiwa na makundi ya kutetea haki za binadamu na wanadiplomasia kwa kutekeleza ukatili mkubwa , ikiwa ni pamoja na mauaji ya zaidi ya raia 2,000 huko El Fasher, jiji kuu la Darfur ambalo kundi hilo liliuteka kutoka kwa jeshi mwezi Oktoba.
Mapigano kati ya jeshi na kundi la RSF yalizuka mwezi Aprili 2023 na yameua maelfu na mamilioni ya watu kuyahama makazi yao, na vita hivyo kuwa moja wapo ya migogoro mbaya zaidi ya kibinadamu kuwahi kuripotiwa duniani.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime