LUKUWI AFANYA ZIARA YA KIKAZI MKOANI MWANZA.

‎‎Naibu Kamishna wa Uhamiaji (Utawala), DCI Elizabeth Lukuwi Oktoba 23 mwaka huu amefanya ziara ya kikazi katika Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mwanza  kwa lengo la kuzungumza na Maafisa na Askari wa Mkoa huo.

‎‎Katika ziara hiyo DCI Lukuwi aliwataka maofisa na Askari wa Uhamiaji kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi, kudumisha nidhamu kazini, na kdumisha ushirikiano kati ya maofisa wa uhamiaji na taasisi nyingine za Ulinzi na usalama.

‎‎Aidha DCI Lukuwi alisisitiza umuhimu wa uwajibikaji, maadili ya utumishi wa umma, na matumizi bora ya teknolojia katika utendaji kazi sambamba na kulinda usalama wa taifa.

‎‎Kwa upande wake Kaimu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza Mrakibu Mwandamizi SSI Jeremiah Mwakibinga alisema kuwa ofisi yake itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi na kushirikiana kikamilifu na makao makuu katika kuhakikisha huduma bora kwa wananchi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii