Tathmini ya elimu ya mwaka wanafunzi wapaza sauti

Wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari wameipongeza Serikali kwa kuboresha miundombinu ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari, wakisema hatua hiyo imeimarisha mazingira ya kujifunza na kufundisha.

Hayo yameelezwa katika Mkutano Mkuu wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Elimu uliofanyika Oktoba 24 mwaka huu jijini Dodoma, Mohammed Saidi kutoka Shule ya Msingi Dodoma, ambaye ni mwanafunzi mwenye mahitaji maalum alisisitiza umuhimu wa kuwajali wanafunzi kama yeye kwa kuwapatia vitabu, viti mwendo, walimu mahiri na kutambua vipaji vyao.

Nenelo Mdachi wa Shule ya Sekondari Viwandani na Zaituni Halfan wa Sekondari Nzuguni walihimiza kushughulikia changamoto za kimaadili miongoni mwa walimu.

Hivyo walisisitiza utekelezaji wa Mwongozo wa Adhafu ili kuimarisha nidhamu, maadili na taaluma shuleni.

Kwa upande wake Mohamod Idi kutoka Sekondari Umonga alitoa wito wa kuongezwa kwa walimu wa Sayansi na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa mkondo wa Amali.

Hata hivyo alisema kuwa mkondo huo unasaidia kukuza maarifa ya vitendo na kuandaa wataalamu wa baadaye.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii