Mawaziri wa ulinzi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya kujihami ya NATO wamekutana Jumatano mjini Brussels nchini Ubelgiji kujadili namna ya kujilinda na kukabiliana na vitisho na uchokozi wa Urusi.
Umoja wa Ulaya unashinikiza kuwepo na mfumo mpya wa kujilinda dhidi ya droni ambao utatakiwa kuanza kufanya kazi kikamilifu ifikapo mwishoni mwa mwaka 2027. Mwezi uliopita, ndege za kivita za NATO zilidungua droni za Urusi zilizokuwa zimeingia kinyume cha sheria katika anga ya Poland.
Hii ni moja kati ya mipango ya Umoja wa Ulaya ambayo itazinduliwa rasmi kesho Alhamisi na inayolenga kuuandaa umoja huo na kile kinachotajwa kuwa kufikia mwaka 2030 kuna uwezekano wa kutokea kwa shambulio la Urusi dhidi ya nchi za Ulaya.