Joseph Kabila ateuliwa kuongoza jukwaa jipya la kisiasa DRC

Mkutano mkubwa wa kisiasa na kijamii juu ya mustakabali wa nchi, ulioitishwa Nairobi, nchini Kenya, na rais wa zamani Joseph Kabila, umezindua jukwaa jipya la kisiasa siku ya Jumatano, Oktoba 15, 2025, liitwalo "le Mouvement sauvons la République démocratique du Congo" (tuokoe Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo). Kulingana na vyanzo vya ndani, mwishoni mwa mkutano, washiriki walimteua Joseph Kabila kama kiongozi wa vuguvugu hili.

Kwa mujibu wa tamko la mwisho la kongamano hili lililotolewa siku ya Jumatano, lengo la vuguvugu hili ni kuchukua hatua kukomesha udikteta na kurejesha mamlaka ya serikali.

Wapinzani hawa wameamua, hasa, kuidhinisha pointi kumi na mbili za kumaliza mgogoro wa DRC zilizopendekezwa na Joseph Kabila katika hotuba yake ya mwisho kwa taifa.

Waliokusanyika Jumanne na Jumatano karibu na rais wa zamani wa Kongo kwa ajili ya "mkutano juu ya mustakabali wa Kongo," viingozi wa kisiasa na kijamii wamefuilia mbali uamuzi wa Mahakama Kuu ya Kijeshi uliomhukumu kifo Joseph Kabila. Kwa mujibu viongozi hao, uamuzi huu ni batili na haukubaliki, kwani unakiuka Katiba na sheria inayosimamia hadhi ya wakuu wa nchi wa zamani.

Washiriki walitoa utambuzi "wa kutisha" wa nchi, wakilaani "mgogoro wenye pande nyingi," kutokana na maoni yao, dhuluma za kisiasa, kiuchumi na kijamii. Wanashutumu serikali ya sasa kwa kukiuka Katiba, kuminya kidemokrasia, na kutumia vyombo vya sheria.

Kongamano hilo linataka kuwepo kwa mazungumzo jumuishi, yanayoungwa mkono na Baraza la Kitaifa la Maaskofu wa Kongo (CENCO) na Kanisa la Kristo nchini Kongo (ECC), kutatua mgogoro huo. Linakataa "mlolongo wowote wa kisiasa" uliopangwa, kulingana na washiriki, na Rais Félix Tshisekedi.

Wanadai kuwa jukwa hili jipya la kisiasa, "Mouvement Sauvons la RDC ," linalenga "kukomesha dhuluma, kurejesha demokrasia, na kukuza maridhiano ya kitaifa."

Vuguvugu hilo limeamua kuanzisha mashambulizi ya kidiplomasia ili kuongeza uelewa miongoni mwa jumuiya ya kimataifa kuhusu mzozo unaosambaratisha DRC na kutaka wanajeshi wote wa kigeni na mamluki waondolewe katika ardhi ya Kongo.

Wakati huo huo, linatoa wito kwa "raia kupinga udikteta ili kuokoa DRC."

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii