Licha ya kuwapatia kombe la Europa League ikiwa ni kombe la kwanza kwa Tottenham Hotspurs kwa miaka 17, kocha Ange Postecoglou amefukuzwa kazi ndani ya klabu hiyo.
Spurs imemaliza nafasi ya 17 kwenye msimamo wa ligi ya England na ametimuliwa siku 16 tu baada ya kuifunga Manchester United na kuchukua Ubingwa wa Europa League.
Postecoglou anatimuliwa baada ya kudumu ndani ya kikosi hicho kwa misimu miwili.
Postecoglou alijiunga na Tottenham Hotspurs tarehe kama ya leo miaka miwili iliyopita 06/06/2023 akitokea Celtic na leo imetimia miaka miwili rasmi.