Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara John Heche pamoja na Katibu Mkuu wa zamani wa chama hicho, Dk Wilbroad Slaa wamewasili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumatatu Mei 19, 2025 kwa ajili ya kufuatilia kesi zinazomkabili Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Tundu Lissu.
Lissu ambaye anakabiliwa na kesi mbili ambazo ni kuchapisha taarifa za uongo kupitia mtandao ya kijamii pamoja na ile ya uhaini.
Kwa mujibu wa uamuzi wa hivi karibuni wa Mahakama mashauri hayo sasa yatasikilizwa kwa mfumo wa mahakama ya wazi (open court) hatua ambayo inawaruhusu wananchi na wadau mbalimbali wa haki kushuhudia mwenendo wa kesi moja kwa moja ndani ya ukumbi wa Mahakama.