Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga kuendelea na kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu leo May 19,2025 ambapo hivi ndivyo hali ilivyo nje ya Mahakama hiyo muda huu saa 12 asubuhi Polisi wakionekana kuimarisha ulinzi.
Lissu anatarajiwa kufikishwa Mahakamani leo baada ya Mahakama kuamuru kuwa afikishwe Mahakamani hapo badala ya kesi kuendeshwa kwa njia ya mtandao kama ilivyokuwa inafanywa hapo awali.
Itakumbukwa Lissu alifikishwa Mahakamani hapo kwa mara ya kwanza April 10, 2025 akikabiliwa na mashtaka ya uhaini na uchochezi ambapo katika shtaka la uhaini, Lissu anadaiwa kuwa April 3, 2025 katika Mkoa na Jiji la Dar es salaam na akiwa Raia wa Tanzania alitengeneza nia ya kuchochea Umma kuzuia uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Ili kupata taarifa zaidi endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya www.jembenijembe.com kupitia Instagram ,Facebook, tikok,x zamani twitter pamoja na YouTube