ZOEZI LA MABORESHO YA DAFTAR LA MPIGA KURA YAENDELEA

 Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Jaji Jacobs Mwambegele ametembelea na kukagua mwenendo wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na uwekaji wazi wa daftari la awali unaoendelea katika mikoa 16 ya Tanzania Bara na  Zanzibar.


Ikiwa vituo alivyotembelea ni katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga na Kibiti mkoani Pwani.

Zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na uwekaji wazi wa daftari la awali ulioanza Mei 16, 2025, bado unaendelea katika mikoa 16 nchini na unatarajiwa kuhitimishwa Mei 22, 2025.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii