Kuwasili kwa Joseph Kabila nchini Kongo Kwapelekea chama cha PPRD matatani

Rais wa Zamani wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo Joseph Kabila amerejea Nchini humo kutafuta Suluhu ya Vita dhidi ya Mzozo wa kisiasa unaendelea.

Inaelezwa kuwa rais huyo wa zamani wa Congo aliwasili Goma usiku wa manane na kupokelewa na kiongozi wa kundi la waasi la AFC/M23, Corneille Nanga.

Kupitia ukarasa wake wa X, Corneille Nangaa amesema kwa pamoja na Kabila wanadhamiria kukomesha kile alichokiita kuwa ni udikteta na migawanyiko nchini Kongo.

Ziara yake huko Goma imechukuliwa kama kitendo cha usaliti wa taifa na  demokrasia huku akihojiwa na televisheni ya taifa msemaji wa serikali ya Kongo Patrick Muyaya amesema kuwa Kabila amepitwa na wakati na alitakiwa kunyamaza.

Aidha amesema kuwa Kuwasili huko kwa Joseph Kabila mjini Goma kunakiweka matatani chama chake cha PPRD ambacho baadhi ya viongozi wake wamekuwa wakihojiwa na mamlaka za Kinshasa huku waziri wa mambo ya ndani akitangaza kusitisha shughuli za chama hicho.

Hata hivyo Ramazani Shadari amesema hawatishiki na hatua hiyo ya serikali."Chama ni katika moyo wa mtu na kichwani mwake. Sisi ni wanachama wa PPRD na tutaendelea kuwa wanachama. Wanachokifanya ni mzaha na mchezo mtupu.

Itakumbukwa kuwa hivi karibuni Kabila alimkosoa Rais Félix Tshisekedi baada ya kumondolewa kinga ya kutoshitakiwa na kueleza kuwa Rais wa Sasa wa Congo amekuwa na uongozi mbaya huku akisema kuwa umelitumbukiza taifa katika mgogoro wa kimuundo na kuifanya Kongo kuwa kichekesho mbele ya jamii na kimataifa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii