KAULI YA JOSEPH MSUKUMA BUNGENI KUHUSU WANAHARAKATI KUTOKA KENYA

Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Musukuma ametoa kauli kali bungeni akilaani matusi na kejeli wanazotupiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan mtandaoni kutoka kwa baadhi ya wanaharakati kutoka nchini Kenya.

Ametoa kauli hiyo wakati akichangia hoja ya bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2025/2026 leo bungeni jijini Dodoma Musukuma amesema si jambo la busara kwa wabunge kukaa kimya wakati kiongozi mkuu wa nchi anadhalilishwa.

Musukuma amesema Tanzania haina ugomvi na wananchi wa kawaida wa Kenya isipokuwa inaugonvi na wanaharakati wa taifa hilo ambao wanatumia mitandao ya kijamii kutoa lugha za matusi dhidi ya Rais Samia na kueleza kwamba Tanzania hakuna cha kujifunza Kenya kutokana na kuwazidi siasa na akiri.

Amesisitiza kuwa Tanzania ni nchi inayojitambua na isiyokubali kuingiliwa au kuchochewa kuvuruga amani yake huku akivitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuendelea kuchukua hatua dhidi ya wanaoeneza chuki na matusi mtandaoni.

Mbunge huyo pia amesema si sawa kwa taifa kuwa na mazingira ambayo mtu anaweza kumdharau Rais wa nchi bila kuchukuliwa hatua, kama ambavyo imekuwa ikifanyika kwenye baadhi ya mitandao kwa kutumia video za kejeli.

Ili kupata taarifa zaidi endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya www.jembenijembe.com kupitia Instagram ,Facebook, tikok,x zamani twitter pamoja na YouTube

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii