DK,TULIA AWANIA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA UYOLE

Siku chache baada ya Mbunge wa Mbeya Mjini Dk Tulia Ackson kutangaza nia ya kugombea ubunge katika Jimbo jipya la Uyole makada wawili wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wameanza kupigana vikumbo Mbeya Mjini huku wengine wakitarajiwa kutia nia muda wowote kuanzia sasa.

Wawili hao wanaopigana vikumbo akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Mbeya Mjini, Afrey Nsomba na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa Charles Mwakipesile.

Vikumbo hivyo vinakuja baada ya Mei 23 mwaka huu Dk Tulia kutangaza upande atakaokwenda kugombea siku chache tangu Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ilipotangaza mgawanyo wa Jimbo la Mbeya Mjini na kuzaa jimbo la Uyole.

Mbali na wawili hao kutangaza nia ya kulitaka jimbo hilo wengine wanaotarajiwa kutupa karata zao katika nafasi hiyo ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Ndele Mwaselela na Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Mbeya, Patrick Mwalunenge.

Awali vigogo hao wenye ushawishi ndani ya CCM walitajwa kuyawinda majimbo ya Rungwe kwa upande wa Mwalunenge kwa kuwa ni nyumbani kwao.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii