CHADEMA MBIONI KUJADILI MUSTAKABALI WA DEMOKRASIA NCHINI

Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika amesema watawala wanatumia mifumo yao kutaka kujaribu kutengeneza vyama mbadala ili kuziba pengo la Chadema la chama kikuu cha upinzani huku akisisitiza kuwa vita hiyo watashinda.

Akizungumza leo Ijumaa Mei 23, 2025, katika kikao maalum chenye ajenda 12 kinachofanyika Makao Makuu ya Chadema Mikocheni-Dar es Salaam Mnyika amesema pamoja na mapigo hayo wanayopitia  lakini bado chama hicho kitashinda na kuwa   cha kihistoria ndani ya chama na Taifa huku akikielezea kikao kuwa sehemu ya kutafakari mustakabali wa Chadema na demokrasia nchini.

Mnyika amesema chama hicho kiko katikati ya vita dhidi ya watawala huku akidai kuna njama za kupinga uamuzi halali wa vikao vya chama na kujaribu kudhoofisha harakati za kudai mabadiliko ya kisiasa nchini  .

“Chama kinapitia wakati mgumu. Tupo katikati ya vita kubwa ya ‘No reforms, no election’ dhidi ya watawala ambao wanakwenda kinyume na matakwa ya wananchi,”

Amedai kuwa Serikali imekuwa ikipinga maamuzi halali ya Baraza Kuu la Chadema lililofanyika Januari 22, 2025, ambalo liliidhinisha uteuzi wa Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na wajumbe wa Kamati Kuu.

“Watawala wanafanya kila jitihada kubatilisha maamuzi ya Kamati Kuu ambayo yalifanyika baada ya uongozi mpya kuingia madarakani. Hii ni vita ya wazi dhidi ya chama chetu,” 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii