UNICEF" Watoto waathirika pakubwa na mzozo wa miaka miwili Sudan"

Idadi ya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto nchini Sudan, kuanzia kwenye mauaji hadi utekaji, vimeongezeka kwa zaidi ya asilimia elfu 1 kufuatia vita ya wenywe kwa wenyewe iliyodumu kwa miaka miwili hivi sasa, limesema shirika linalohudumia watoto UNICEF.

Katika taarifa yake, UNICEF inasema vitendo hivyo awali vilikuwa vinaripotiwa tu katika maeneo mawili ambapo mashambulio yameonekana kutekelezwa dhidi ya shule na majengo ya hospitali.

Hata hivyo kutokana na kuongezeka kwa mzozo kati ya jeshi la serikali na wapiganaji wa RSF, ukiukaji wa haki za watoto umeripotiwa pia katika maeneo mengine ya Sudan.

Lakini kutokana na kuongezeka kwa mzozo kati ya jeshi la serikali na wapiganaji wa RSF, ukiukaji wa haki za watoto umeripotiwa pia katika maeneo mengine ya Sudan.

Ripoti ya UNICEF pia inaonyesha kwamba idadi ya watoto waliouawa nchini Sudan iliongezeka kutoka kwa 150 mwaka wa 2022 hadi 2,776 katika mwaka wa 2023 na 2024, idadi ambayo inahofiwa kuwa huenda zikaongezeka.

Mashambulio dhidi ya shule na hospitali pia yakiripotiwa kuongezeka kutoka 33 mwaka wa 2022 hadi 181 katika mwaka wa 2023 na 2024.

Vilevile idadi ya watoto wanaohitaji misaada ya kibinadamu imeongezeka kutoka Milioni 7.8 mwazoni mwa mwaka wa 2023 hadi zadi ya Milioni 15.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii