Shambulizi hilo limeorodheshwa kuwa baya zaidi kuwahi kutokea shuleni kwenye historia ya Sweden. “Takriban watu 10 wameuwawa leo,” Mkuu wa polisi Roberto Eid Forest aliambia wanahabari, akiongeza kuwa polisi hawangeweza kutoa idadi kamili kutokana na idadi kubwa ya watu waliyojeruhiwa.
Polisi hawakutoa taarifa zozote kuhusu watu waliokufa wala umri wao, na iwapo walikuwa wanafunzi au walimu kwenye shule ya upili ya Risbergska. Vyombo kadhaa vya habari vimeripoti kuwa mshambuliaji alijipiga risasi pia, ingawa polisi hawakudhibitisha hilo.
“Mshukiwa huyo hajulikani kwa polisi, na wala hahusishwi na kundi lolote la kihalifu,” Forest alisema, akiashiria mashambulizi ya risasi pamoja na mabomu ambayo yameshuhudiwa Sweden katika miaka ya karibuni. Hata hivyo amesema kuwa hawatarajii mashambulizi zaidi ndani ya Sweden.