Hii ni mara ya kwanza kwa rais wa Kongo kuzungumza tangu mashambulizi ya waasi katika siku za hivi karibuni mashariki mwa nchi hiyo, huko Goma. Wakati wa hotuba yake kwa taifa, rais wa Kongo ametangaza kwamba "mashambulizi haya ni kosa kwa historia yetu" na kwamba "jibu kali linaendelea", anaripoti mwandishi wetu huko Kinshasa, Patient Ligodi. Hotuba yenye maneno makali, iliyotolewa kwa sauti nzito na ya taadhima. Félix Tshisekedi ameonekana yuko tayari kwa vita.
Félix Tshisekedi pia amesisitiza juu ya chaguo la kidiplomasia: "Tumechukua hatua muhimu. Tunapendelea njia ya mazungumzo."
Raids wa DRC wa nchi ametoa wito kwa uhamasishaji wa jumla. "Vita hivi ni vya watu wote. Katika maeneo yetu, tuunganishe juhudi zetu,” amesema. Pia ametangaza kuzindua mpango wa dharura wa kibinadamu na kuwataka wakazi kupambana kwa ujasiri na kuwa watulivu.
Kwa upande wa usalama, amehakikisha kuwa hatua zimechukuliwa. "Hatujabaki kimya," amejitetea. Na akaongeza: "Mfumo wa usalama umeimarishwa."
Félix Tshisekedi pia ameoa heshima kubwa kwa askari na wapiganaji waliofariki vitani: "Ninapongeza ujasiri wa jeshi letu, wazalendo wetu, walinda amani wetu na askari waliofariki vitani."
Rais wa Kongo ameinyooshea tena kidole cha lawama Rwanda, akishutumu uwepo wa maelfu ya wanajeshi wa Rwanda katika ardhi ya Kongo na kuwaita M23 "kibaraka". Ameshutumu "ukiukaji wa wazi wa katiba ya Umoja wa Mataifa" na "kudharau maadili ya ulimwengu" , huku akisema, "tutapigana."
Pia ametangaza hatua za kiuchumi, ikiwa ni pamoja na maagizo kwa serikali kupunguza gharama za maisha ya taasisi na kutoa wito kwa sekta binafsi kuunga mkono juhudi za vita.
Hatimaye, ametoa wito wa kuandikishwa kwa vijana katika jeshi na kuhitimisha: "DRC haitasalimu amri. Sitakuacheni kamwe."