AJIFUNGUA MTOTO MWENYE VICHWA VIWILI

Mkazi wa kijiji cha Chonga, wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Lillian Ismail, mwenye umri wa miaka 21, amejifungua mtoto wa kiume akiwa na vichwa viwili. Tukio hilo limeacha jamii ya kijiji hicho katika mshangao mkubwa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mashuhuda, Lillian alijifungua kwa njia ya upasuaji kwenye hospitali ya wilaya ya Nkasi na baadae kupewa rufaa kwenda hospitali ya rufaa ya mkoa Sumbawanga ambapo alilazwa kwa muda wa siku tano, nako wakamshauri kwenda hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya kwa matibabu zaidi ambako ameshindwa kwenda kwa kushindwa kumudu gharama baada ya kukosa fedha za matibabu na usafiri.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii