Mwanafunzi huyo Mahmoud Khalil alikamatwa Jumamosi na maafisa wa wiraza ya Marekani ya usalama wa ndani kwenye makazi ya chuo kikuu, chama cha wanafunzi wa chuo kikuu cha Columbia kilisema katika taarifa.
Kushikiliwa kwa Khalil inaonekana kama mojawapo ya juhudi za kwanza za Rais Trump, kutimiza ahadi yake ya kutaka kuwafurusha baadhi ya wanafunzi wa kigeni waliohusika katika vuguvugu la maandamano ya kuiunga mkono Palestina.
Shambulizi la Hamas la Oktoba 7, 2023 dhidi ya Israel na shambulizi lililofuata la Israel huko Gaza lilichochea miezi kadhaa ya maandamano ya Wapalestina katika vyuo vikuu vya Marekani.
Mke wa Khalil ni raia wa Marekani na Khalil ana kibali cha mkazi wa kudumu, chama cha wanafunzi kimesema.