Saudi Arabia kuwa mwenyeji wa mkutano wa maandalizi ya mkutano wa Trump na Putin kuhusu Ukraine

Saudi Arabia itakuwa mwenyeji wa mkutano wa maandalizi kati ya maafisa wakuu wa Urusi na Marekani siku ya Jumanne, Februari 18, kabla ya mkutano wa kilele kati ya marais wa Urusi na Marekani kuhusu Ukraine, chanzo kilicho karibu na serikali ya Saudi Arabia kimeliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumatatu. 

Mshauri wa masuala ya usalama wa taifa wa rais wa Marekani, Mike Waltz, na mjumbe maalum wa Mashariki ya Kati, Steve Witkoff, wataiwakilisha Marekani, chanzo kimesema.

Nchi hiyo ya Kiarabu itaandaa mkutano wa maandalizi kati ya maafisa wakuu wa Urusi na Marekani siku ya Jumanne kabla ya mkutano wa kilele kati ya marais wa Urusi na Marekani kuhusu Ukraine.

Washington inathibitisha mkutano na Urusi mjini Riyadh siku ya Jumanne

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, Mshauri wa masuala ya Usalama wa taifa Mike Waltz na Mjumbe Maalumu wa Mashariki ya Kati Steve Witkoff watawakilisha Marekani katika mkutano na Urusi mjini Riyadh siku ya Jumanne, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema Jumatatu.

Maafisa hao watatu wa Marekani "watakutana na ujumbe wa Urusi mjini Riyadh siku ya Jumanne," msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Tammy Bruce meisema. Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov na Yuri Ushakov, mshauri wa masuala ya kidiplomasia wa Vladimir Putin, wanatarajiwa kwenda Riyadh siku ya Jumatatu kwa mkutano huo, ofisi ya rais wa Urusi imesema.

Volodymyr Zelensky kuzuru Saudi Arabia siku ya Jumatano

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky atafanya ziara nchini Saudi Arabia siku ya Jumatano, siku moja baada ya mazungumzo ya Urusi na Marekani mjini Riyadh, msemaji wake ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumatatu.

"Ni ziara rasmi ambayo imepangwa kwa muda mrefu," ameongeza Serguiy Nykyforov, bila kutoa maelezo zaidi. Ukraine inaendelea kukabiliwa na mashambulizi ya Urusi kwa muda wa miaka mitatu, ambao utawala mpya wa Marekani umeahidi kuumaliza.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii