Kiwanda cha mafuta Libya chafungwa

Kiwanda kimoja cha kusafisha mafuta cha Libya kilichopo magharibi mwa Libya kimefungwa baada ya mapigano kati ya makundi yenye silaha kuzuka mapema Jumapili na kusababisha moto kwenye miundombinu, kampuni ya mafuta ya serikali NOC imesema.

Vifaru kadhaa katika kiwanda cha kusafisha mafuta cha Zawiya, mji ulioko kilomita 45 magharibi mwa Tripoli na moja pekee magharibi mwa Libya ambacho kwa ajili ya soko la ndani la mafuta, kilishika moto, kwa mujibu wa video zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii kabla ya moto kudhibitiwa.

Kiwanda cha Zawiya kilichojengwa 1974, kipo katika mji wa bandari na kituo cha kuagiza na kusafirisha mafuta, ndicho kikubwa zaidi baada ya kile cha Ras Lanouf, chenye uwezo wa kusafisha mapipa 120,000 kwa siku.

NOC ilitangaza katika taarifa yake kusimamishwa kwa uzalishaji, kutokana na hali ya hatari ya kiwango cha juu cha tatu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii