Kwa miongo sasa, wanadamu wamekuwa wakikusanyika kwa vikundi
vidogo kula chakula pamoja. Kwa nini ni muhimu – na kwa nini tunaendelea na
mila hii?
Kula chakula pamoja ni jambo la kawaida sana kwa wanadamu.
Mikusanyiko ya chakula na marafiki, sherehe za chakula, na mikusanyiko ya
likizo ambapo mara nyingi tunajizidisha – kula chakula pamoja ni jambo
linalofanyika kila siku, kiasi kwamba mara nyingi halizingatiwi isipokuwa pale
ambapo watu wanahisi kuwa halitendeki vya kutosha, jambo ambalo linaweza kuwa
na umaarufu kwa wakati mwingine.
Ni hofu kubwa kuhusu kupungua kwa mikusanyiko ya familia kwa
chakula, kwa mfano, mara nyingi hugonga vichwa vya habari.Kula pamoja,
inaonekana, si jambo la kawaida tu, bali ni jambo lenye nguvu kubwa. Lakini kwa
nini?
Kula chakula kwa pamoja inaweza ikaturudisha nyuma enzi zile
za asili ya spishi yetu. Sokwe na bonobo, ndugu zetu wa karibu zaidi mamalia wa
hali ya juu pia hula kwa pamoja na makundi yao ya kijamii.
Hata hivyo, kusaidia watu na chakula si sawa na kula pamoja,
anasema mwana-sosholojia Nicklas Neuman kutoka Chuo Kikuu cha Uppsala, Sweden.
“Unaweza kugawa chakula kama bidhaa bila kukaa chini na kula na wengine,”
anasema. Wanadamu wanaonekana wameongeza na kujenga desturi kwenye shughuli hii
ya kula kwa pamoja.
Ingawa hakuna anayejua kwa hakika ni lini wanadamu au mababu zetu walijifunza kupika, ikakadiriwa ilianza miaka milioni 1.8.
Hata hivyo, wakati mtu anapojitahidi kuwinda au kukusanya
chakula, kuwasha moto, na kupika, inaonyesha kuwa alikuwa na kundi la kijamii kumsaidia
katika hatua zote za maandalizi ya kupika chakula.
Pindi mnapokaa karibu na Moto ,huku giza likitanda
,utagundua kuwa unapendelea kukaa muda mrefu zaidi.
Robin Dunbar, mtaalamu wa antropolojia kutoka Chuo Kikuu cha
Oxford, anaamini kuwa masaa hayo ya ziada yanaweza kuwa fursa muhimu ya
kuimarisha uhusiano wa kijamii kwa kula pamoja.
Utafiti wa Dunbar ulionyesha kuwa kula chakula na wengine
mara kwa mara kunahusiana na kuridhika zaidi maishani na kuwa na marafiki wa
kutegemea msaada.
Utafiti huo ulionyesha kuwa mikusanyiko ya chakula ni chanzo
cha athari za kijamii, na si matokeo ya hizo athari.
“Kula chakula huamsha mfumo wa endorfinu wa ubongo, ambao
unaoana kati ya wanadamu na mamalia wa hali ya juu,” anasema Dunbar.
“Kula pamoja kama kundi kunaimarisha athari hii ya endorfinu
kwa njia ile ile kama vile kufanya mazoezi pamoja. Hii inatokea kwa sababu
shughuli zinazofanyika kwa wakati mmoja huongeza uzalishaji wa endorfinu
maradufu.”
Kula chakula kilekile kwa wakati mmoja na mtu mwingine
hufanya mtu huyo kuwa na uaminifu zaidi. Utafiti uliofanywa na waandishi wa
habari Cynthia Graeber na Nicola Twiley katika podcast yao Gastropod ulionyesha
kuwa katika mfano wa uwekezaji, watu walitoa fedha zaidi kwa mtu waliyekula
pipi sawa na yeye hapo awali.
Vile vile, watu waliokula vibanzi sawa walikuwa haraka
kuafikiana kwa mazungumzo kuliko wale waliokula vibanzi tofauti.
Ayelet Fishbach kutoka Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha
Chicago aligundua kuwa ladha zinazofanana katika chakula zinaweza kuwa ishara
ya maadili yanayoshirikiana, ingawa hii ni jambo linaloweza kutofautiana kwa
wakati wa sasa.
Hata hivyo, kula pamoja si kitendo kilicho na athari chanya
kila mara. Sherehe za chakula, ambapo chakula kingi kinashirikishwa, zinaweza
kuwa njia za kuonyesha mamlaka au udhibiti.
Hebu fikiria desturi ya mavuno abapo mkulima hutoa mlo
mwimgi kwa wafanyakazi wake, au sherehe ya ofisini ambapo ukarimu wa mwajiri,
au ukosefu wake, unachunguzwa na waliohudhuria.
Mikusanyiko ya chakula ya familia, ingawa inasifiwa, si
lazima iwe bila migogoro.
“Watu wanasema wanapenda kula chakula na marafiki na
wapendwa. Lakini inaweza pia kuwa ni uzoefu mbaya kula pamoja na wapendwa,”
anasema Neuman. “Ni mahali pa kudhibiti na kutawala pia.”
Kula kwa pamoja ambapo mtu anakosoa uamuzi wako au uzito wa
mwili wako ni eneo ambalo halikusaidii maishani.
Katika utafiti mwingine unaohusu mtazamo wa wazee nchini Sweden, Neuman aligundua jambo la kushangaza.
“Tuliwauliza kwa makusudi kama wanahisi kudhuriwa na kula
peke yao. Wengi wao hawaoni shida,” anasema. Wanapenda kula na wenzao, lakini
wengi wao hawahisi upungufu wa hilo kama vile ungetarajia. Pengine hili
linahusiana na hali ya upweke, anadhania: kama mtu anajihisi upweke, basi kula
peke yake huenda kukaongeza usumbufu.
“Lakini kama wewe ni mtu ambaye mara kwa mara unakula na
wengine, basi pengine, wakati mwingine,” anasema Neuman, “itakuwa vizuri kukaa
peke yako na kusoma kitabu.”