Tambua umuhimu wa Efeso 4:2-3 katika kulinda amani na umoja wa kisiasa Tanzania

Tanzania kwa muda mrefu imekuwa mfano wa utulivu na mshikamano katika Afrika mashariki. 

Hata hivyo ,kama ilivyo katika mataifa mengine yanayotumia mifumo ya demokrasia ,chaguzi ,mijadara ya kisera ,natofauti za kiitikadi  huwa zinaibua misuguano ya kijamii na kisiasa .

 Katika mazingira haya maandiko ya kiroho yanaweza kuwa dira ya maadili yanayoongoza tabia,mawasiliano na maamuzi yetu.

Kifungu cha Efesso: 4: 2-3 kinasema" Muwe wanyenyekevu na Wapole, wenye uvumilivu,mkivumiliana ninyi kwa ninyi kwa upendo.

Jitahidi kulinda umoja na roho kwa kifungo cha amani".

Maneno  haya yanatoa mwongozo muhimu ambao unaweza kutumika katika kudumisha amani,kuheshimiana ,na umoja katika mazingira ya kisiasa ya Tanzania.

1: Unyenyekevu: Msingi wa mazungumzo ya kidemokrasia. 

Moja ya changamoto kubwa katika siasa ni majigambo na kujiona sahihi kupita kiasi ,unyenyekevu unaotajwa katika Efesso 4:2-3  ni mwito kwa viongozi na wananchi kutambua kuwa:

* Hakuna chama kilicho na majibu ya masuala ya yote.

* Hakuna mwanadamu asiyeweza kukosea.

* Kila upande unaweza kujifunza kutoka kwa mwingine.

Unyenyekevu  hujenga mazingira ya kusikilizana ,tofauti na mazungumzo yenye kelele ,maneno makali,au  kupishana kauli kunakoshuhudiwa mara kwa mara katika mijadara ya kisiasa.

2: Upole: Dawa dhidi ya lugha za uchochezi.

Upole hauimanishi udhaifu ,ni uwezo wa kutawala hisia hata pale ambapo mtu ana hoja nzito,hili lina umuhimu mkubwa katika kipindi cha:

* Kampeini za kisiasa.

* Majadiliano  ya Bungeni.

* Mijadara kwenye mitandao ya kijamii.

* Mikutano ya hadhara.

Upole huzuia  lugha za matusi ,kejeli na maneno ya uchochezi ambayo yanaweza kuibua migawanyiko.

Kwa Tanzania taifa lenye historia ya undugu na mshikamano ,upole ni nguzo ya kuzuia migogoro isiyo ya lazima.

3: Uvumilivu: Kukubali tofauti bila kugombana:Efesso 4: 2 inasisitiza uvumilivu. Kiungo muhimu katika jamiiya kidemokrasia Tanzania ina:

* Makabila zaidi ya 120.

* Dini mbalimbali.

* Mitazamo tofauti ya kiuchumi na kisiasa.

Katika mazingira haya,kutofaitiana ni kawaida ,uvumilivu utukumbusha kwamba: 

*Tofauti za kisiasa hazitufanyi kuwa maadui.

*Mawazo mengine yanaweza kuwa na faida kwa taifa.

*Kila mtu ana haki ya kuamini anachoamini,ilimradi hatumii imani hiyo kuumiza wengine.

4; Kuvumiliana kwa upendo: Kuondoa chuki katika siasa.Siasa maranyingi hujenga mitazamo isiyo rafiki kama sisi dhidi yao."Lakini Biblia inaagiza " kuvumiliana kwa upendo".ikiashiria: 

* Kuhshimu utu wa kila mtu hata kama hatuungi mkono msimamo wake.

* Kuepuka chuki,hasira na roho ya visasi.

* Kupinga propaganda  zinaleta hofu na mgawanyiko.

Katika Tanzania ,ambako jamii nyingi huishi kwa ukaribu na mshikamano  wa kijamii bila kujali msimu wa kisiasa.

5: Kulinda umoja wa kitaifa: Kipaumbele zaidi ya itikadi.Neno" Jitahidini" linamaanisha kuwa umoja hauji kwa bahati unahitaji kazi,juhudi na nia thabiti.

Katika kipindi cha malumbano ya kisiasa iwe ni uchaguzi ,sheria mpya ,au mijadara mikali ,wananchi na viongozi wanaweza kuiweka nchi katika hatari ya: 

* Migawanyiko ya kisera.

* Manung'uniko yasiyoisha.

* Kuzuka kwa misuguano ya kijamii.

Umoja wa kitaifa ni raslimali adimu ambayo Tanzania imejengwa kwa miaka mingi ,Effeso 4:3 inaonya kuwa umoja huo ni " kifungo cha amani"yaani bila umoja,amani inalegalega.

Kwa hiyo,kila mtanzania,awe kiongozi ,mwanachama wa chama chochote ,au mwananchi wa kawaida,anapaswa kuuliza: Je,kauli yangu,au hatua yangu inalinda umoja au inabomoa?

6:Amani: Matokeo ya Tabia zetu.Amani si mwongozo tu wa kisiasa,bali ni thamani ya kiroho . 

Aidha amani inajengwa kila siku kupitia.

* Kauli zetu.

* Mitazamo  yetu.

* Mawasiliano yetu.

* Mienendo yetu.

 Katika Tanzania ambako changamoto za kiuchumi ,kijamii na kisiasa zimeongezeka,amani inazidi kuwa kuna umuhimu.Maandiko ya Effesso 4:2-3 yanatoa mwito wa kuishi kwa namna inayochochea.

* Majadiliano ya Busara.

* Uongozi wa hekima.

* Ujirani mwema.

* Utamaduni wa kusameana.

 Haya yote  huchangia Tanzania yenye utulivu na maendeleo endelevu.

Kwa kuzingatia hali ya sasa nchini Tanzania. Effesso 4:2-3 si tu kifungu cha dini : ni dira ya maadili inayoweza kuongoza taifa katika kudumisha amani,mshikamano  na ustaarabu wa kisiasa.

Ikiwa viongozi ,wafuasi wa vyama,na wanachi wote watapokea ujumbe huo katika mioyo yao,Tanzania itaendelea kuwa taifa lenye umoja,busara na mazungumzo ya kuvutia baadala ya migawanyiko na manung'uniko .

Itakumbukwa kuwa ni mwaliko kwetu sote.

Tudumishe Unyenyekevu, upole ,uvulivu upendo,na umoja kwa manufaa ya Taifa na vizazi vijavyo.

Na@Mbeki Mbeki.

Kagera.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii