Muhudumu wa Hotel Ahusishwa Kumuwekea DAWA za Kulevya Marehemu Mwanamuziki Liam Payne

Mamlaka mjini Buenos Aires inaendelea na uchunguzi wao kuhusu kifo cha nyota wa zamani wa #OneDirection #LiamPayne, Wanashuku kuwa mfanyakazi wa hoteli huenda alimpa dawa za kulevya kabla ya kuanguka kwa bahati mbaya kutoka kwenye balcony ya ghorofa ya tatu ya CasaSur Palermo.

Mfanyakazi huyo anashukiwa kumpa #Payne dawa ya kupunguza wasiwasi ambayo iligunduliwa katika chumba chake baada ya kifo chake.

Kulingana na TMZ, uchunguzi unalenga hasa ikiwa mfanyakazi wa hoteli alihusika katika kutoa baadhi ya dawa zinazopatikana katika mfumo wa mwimbaji huyo, Dawa hizi zilijumuisha mchanganyiko wa crack, cocaine, ketamine, ecstasy.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii