Rais Paul Biya arejea nchini baada ya wiki saba za kutokuwepo na kuzua wasiwasi

Rais wa Cameroon Paul Biya amerejea nchini Tangu siku ya Jumatatu Oktoba 21, 2024. Aliwasili kwenye uwanja wandege wa kimataifa wa Yaounde saa 12: 38 za za Cameroon, kulingana na picha zilizorushwa hewani na televisheni ya serikali, CCRTV. 

Paul Biya, 92, rais wa Cameroon kwa miaka 42, alikuwa nje ya nchi kwa wiki saba, na hali yake ya afya ilizua wasiwasi, huku mamlaka ikisema ni habari za uongo na mawasiliano tofauti kutoka kwa serikali. 

Baada ya ndege ya rais kutua, Paul Biya alirekodiwa, akiwa na mkewe, akisalimiana na viongozi waliofika kumkaribisha, huku umati wa watu wenye furaha ukimsubiri mbele ya jengo. Katika picha hizo, alionekana Mkuu wa Nchi, akiwa amevalia suti ya bluuakizungumza na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Waziri wa Nchi, Ferdinand Ngoh Ngoh. Mazungumzo hayo yalichukua dakika chache kabla ya Rais Biya kuingia ndani ya gari ambalo lilimpeleka hadi ikulu ya rais, bila kutoa tamko ama kwa umati au kwa televisheni. Siku ya Jumatatu jioni, Paul Biya alikuwa katika vyumba vyake vya kibinafsi katika jengo hili, anaripoti mwandishi 

Kwa mamia ya wanaharakati kutoka RDPC, chama chake, walikusanyika karibu na uwanja wa ndege na ambao walisubiri kwa saa nyingi, wakiimba nyimbo za kumsifu Paul Biya, alipunga mkono kutoka kwa dirisha lililoshushwa la gari lake. Kando ya kilomita 25 zinazotenganisha uwanja wa ndege na ikulu ya rais na njia panda kuu za mji mkuu zilizopambwa kwa mabango ya kumtakia "karibu tena" kwa Kifaransa na Kiingereza, umati wa watu wenye shauku walikuwa wamekusanyika, wakiwa na shauku ya kumuona yule ambaye hayupo kwa muda mrefu, hali ambayo katika wiki za hivi karibuni ilisababisha uvumi mwingi wa kutisha.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii