Raia wa Somaliland, eneo lililojitenga na Somalia wanashiriki uchaguzi mkuu

Wakaazi wa jimbo la Somaliland, lililojitenga na Somalia miaka 33 iliyopita, wanapiga kura leo kumchagua rais, kipindi hiki kukiwa na msukosuko wa kidiplomasia kai ya utawala wa Mogadishu na nchi jirani ya Ethiopia, iliongia mkataba wa kibiashara na usalama na jimbo hilo.

Tangu mwaka 2003, wakaazi wa jimbo la Somaliland, wamekuwa wakishiriki kwenye uchaguzi wa kumchagua rais na wabunge wao.


Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya jimbo hilo linawapiga kura Milioni 1 waliondikishwa, na wanatarajiwa kushiriki kwenye uchaguzi huo, kumchagua rais atakayewatumikia kwa miaka mitano ijayo.

Wagombea watatu wanatafuta uongozi wa jimbo hilo, akiwemo rais wa sasa Muse Bihi Abdi, anayetaka muhula wa pili.

Mpinzani wake mkuu ni Abdirahman Mohamed Abdullahi, maarufu kwa jina la ‘‘Irro”. Uchaguzi huu unaangaliwa na mashirika mbalimbali ya kimataifa yanayohimiza uongozi bora na demokrasia.

Uchaguzi huu ni muhimu kwa Somaliland ambayo inaendelea kutafuta kutambuliwa na dunia kama nchi huru,inayoweza kujiongoza lakini pia inalenga kuonesha kuwa, inadumisha demokrasia.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii