Ndege ya kubeba Mbwa nauli kuanzia Mil. 1.5

Kuna ndege za Abiria, ndege za mizigo alafu kuna ndege za Mbwa kwa kifupi wamiliki wa Mbwa Nchini Marekani hawatoteseka tena pale wanapotaka kusafiri na Mbwa wao kwa kutumia usafiri wa ndege baada ya Shirika la ndege liitwalo BARK AIR kuanzisha huduma ya kusafiririsha Mbwa na wamiliki wake.

Kutokana na Safari yake ya kwanza mwezi uliopita, Shirika hilo limeona uhitaji mkubwa wa wamiliki wa Wanyama wanaotamani kusafiri na Mbwa wao na kutangaza kuongeza safari za miji mingine mitano ukiachia mbali zile za awali kati ya New York (HPN) na Los Angeles (VNY) pamoja na New York (HPN) na London (BQH) nchini Uingereza.

Bark Air imetangaza ongezeko la ruti mpya kuelekea Paris nchini Ufaransa (LBG), Chicago (MDW), San Francisco/San Jose (SJC) Phonenix (PHX) na Miami/Fort Lauderdale (FXE), nchini Marekani ambapo Mbwa yeyote anaweza kusafiri katika ndege hii huku akipatiwa  huduma kama za Binadamu ikiwemo chakula na malazi lakini kwa sharti moja tu kila Mbwa amepatiwa chanjo zote stahiki na makaratasi na vibali halali vya kusafiria.

Abiria wote ambao ni Binadamu lazima wawe na umri kuanzia miaka 18 na kuendelea huku tiketi za ndege zikianzia kuuzwa kuanzia $6000 (Tsh Milion 15.7) kwa Mbwa mmoja na binadamu mmoja kati ya New York na Los Angeles huku nauli ikiwa ni $8000 (Tsh Milioni 20.9) kati ya New York na London ndani ya ndege hiyo ya tiketi 10 pekee kwa safari moja (zinazojumuisha mbwa mmoja na Binadamu)

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii