Marekani yaipiga marufuku kampuni kubwa ya mawasiliano ya China kwa madai ya ujasusi

Kampuni ya Unicom ya China imekuwa kampuni kubwa ya hivi punde zaidi ya mawasiliano ya simu nchini China kupigwa marufuku kutoka Marekani kwa sababu ya wasiwasi "muhimu" wa usalama wa taifa na ujasusi.

Tume ya Mawasiliano ya Shirikisho (FCC) ilisema kuwa imepiga kura kwa kauli moja kubatilisha idhini kwa kitengo cha kampuni ya Marekani kufanya kazi nchini Marekani.

Ni lazima kampuni iache kutoa huduma za mawasiliano ya simu nchini Marekani ndani ya siku 60.

Tangazo hilo linakuja baada ya mpinzani wake mkuu China Telecom kunyang'anywa leseni yake ya kufanya kazi nchini Marekani mwezi Oktoba.

Mwenyekiti wa FCC Jessica Rosenworcel alisema katika taarifa yake: "Kumekuwa na ushahidi unaoongezeka - na pamoja na hayo, wasiwasi unaoongezeka - kwamba wabebaji wanaomilikiwa na serikali ya China ni tishio la kweli kwa usalama wa mitandao yetu ya mawasiliano."

Katika taarifa iliyotumwa kwa barua pepe kwa BBC, China Unicom ilisema kitengo chake cha Marekani "kina rekodi nzuri ya kuzingatia sheria na kanuni husika za Marekani na kutoa huduma za mawasiliano ya simu na masuluhisho kama mshirika wa kuaminika wa wateja wake katika miongo miwili iliyopita".

"China Unicom (Hong Kong) Limited itafuatilia kwa karibu maendeleo ," iliongeza.

Ubalozi wa China mjini Washington haukujibu mara moja ombi la maoni yake kutoka kwa BBC.

Makampuni ya teknolojia na mawasiliano ya simu ya China yakifuatiliwa katika miaka ya hivi karibuni na mamlaka ya Marekani juu ya masuala ya usalama wa taifa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii