Raila Odinga Kutangaza Alhamisi Siku ya kurejeshwa.Kwa Maandamano

Kiongozi wa upinzani na kinara wa muungano wa Azimio Raila Odinga amesema kuwa Alhamisi ataweka wazi mstakabali wa muungano wake kuhusiana na urejeo wa maandamano kote nchini. 

Katika taaarifa aliyoitoa katika ofisi yake eneo la Upper Hill kiongozi wa Azimio alionekana kughadhabishwa kwake na utendakazi wa serikali ya Kenya Kwanza na kusema kuwa Wakenya wawe tayari kwa mwelekeo mwingine. 

Raila alizungumza wakati ambapo kinara mweza wa muungano huo Martha Karua alimshtumu Rais William Ruto kwa kupendekeza mswada ambao kulingana nae ulikuwa ni kuwakandamiza wafanyabiashara wadogo kutoka Mlima Kenya. 





Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii