Mhubiri Mackenzie awadai Wanahabari mgao wake

Mhubiri tata, Paul Mackenzie anayedaiwa kuchangia vifo vya watu wengi katika msitu wa Shakahola, amewataka Wanahabari kumnunulia mkate na maziwa akisema wametengeneza pesa nyingi kupitia jina lake. 

Mackenzie ameyasema hayo mbele ya Wanahabari mwishoni mwa wiki wakati alipofikishwa katika Mahakama ya Shanzu kusikiliza sharuri la mashitaka linalomkabili.

“Mmetengeneza pesa sana kwa jina yangu lakini hamninunulii hata paketi ya maziwa. Si mninunulie na mimi hata paketi ya maziwa,” alisema Mackenzie kitu kauli qmbayo iliwafanya baadhi ya Wanahabari kuangua kicheko huku wakimjibu kwamba, “usijali tutakununulia tu.”

Pastor Mackenzie, mkewe na watu wengine 16 walikuwa wamefikishwa katika mahakama hiyo ambapo upande wa mashtaka uliomba kupewa siku 60 zaidi za kuendelea kumzuilia mhubiri huyo tata, ili kukamilisha uchunguzi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii