Afisa Manunuzi awekwa ndani Manyoni

Mkuu wa mkoa wa Singida Peter Serukamba amemsweka ndani afisa manunuzi wa halmashauri ya Manyoni Joseph Swila  kwa kukiuka maagizo aliyoyatoa jana wakati alipofika kukagua ujenzi wa wodi ya wanawake, wanaume na chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya Manyoni.


RC Serukamba alimuagiza mhandisi wa halmashauri na afisa manunuzi kuongeza mafundi ili kuongeza kasi ya ujenzi ambapo unatakiwa kukamilika kabla ya June 30 mwaka huu

Mara baada ya kufika kuona utekelezaji wa agizo Serukamba amekerwa na afisa manunuzi Joseph Swila kwa kuonekana kumtetea  mkandarasi anayejenga Majengo hayo huku akiwa hapatikani kwenye simu na hayupo  site 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii