Mkulima apigwa risasi Simanjiro

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Walter Kaaya (34) mkazi wa Simanjiro mkoani Manyara amenusurika kifo kwa kupigwa risasi na Paulo Laizer (43) mfugaji wilayani humo kufuatia mzozo wa mifugo kukutwa shambani ikiharibu mazao.


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara RPC George Katabazi amesema majeruhi alikuwa akiondoa ng'ombe hizo kwenye shamba lake la ekari 200  zilizokuwa na mazao mbalimbali yakiweno mahindi na maharagwe

Wakati anaziondoa ng'ombe shambani mtuhumiwa alifika na kuibua mzozo na kuchukua silaha yake aina ya bastola na kumpiga risasi begani 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii