Jumla ya maduka 21 kati ya 110 yanayomilikiwa na wafanyabiashara mbalimbali ambayo ni mali ya jumuiya ya Wanawake wa chama cha mapinduzi (CCM UWT) Wilaya ya Njombe yameteketea kwa moto na kusababisha hasara kutokana na mali kuungua

Moto huo umetokea majira ya saa tatu usiku wa Aprili 1 mwaka huu ambapo Mkaguzi Loti Madauda kwa niaba ya Kaimu Kamanda wa  jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Njombe amesema walipata taarifa ya moto huo majira ya  saa tatu na dakika 28 na kufika saa tatu na dakika 31 na kuanza zoezi la uzimaji moto huo mpaka majira ya saa saba usiku.

Aidha Katibu tawala Wilaya ya Njombe Emmanuel George amesema chanzo cha awali cha moto huo ni hitilafu ya umeme huku uchunguzi wa kina ukiendelea kufanyika na kisha itatolewa taarifa zaidi.

Kwa upande wake katibu wa CCM mkoa wa Njombe Julius Peter amelipongeza jeshi la zimamoto na uokoaji pamoja na wananchi kwa kujitokeza kuzima moto huo pamoja na kuokoa mali mbalimbali za wafanyabiashara huku akiwaomba wafanyabiashara kutulia wakati tathmini ya maafa itakapofanyika.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii