Makamu wa Rais wa Marekani ziarani Tanzania

Makamu wa Rais wa Marekani kamala Harris ameanza rasmi ziara yake ya nchini Tanzania ambapo hii leo anatarajiwa kufanya mikutano na viongozi wa serikali wakiongozwa na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan.


Kamala aliwasili mjini Dar es salaam jana usiku akitokea Ghana, na kulakiwa na Makamu wa Rais Dr Philip Mpango pamoja na viongozi wengine wakuu wa serikali. 

Kando na mazungumzo yatayolenga kuimarisha ushirikiano wa nchi hizo mbili, mwanadiplomasia huyo wa ngazi za juu Marekani atatembelea Makumbusho ya Taifa na kumbukumbu ya ulipuaji wa Ubalozi wa Marekani mjini humo.

Kadhalika atakutana na wajasiriamali, ambapo Marekani imekuwa ikiendesha miradi kadhaa ya kuhamasisha kuinua pato la wananchi hasa wanawake na vijana kupitia kila sekta. Ziara ya Kamala Afrika inatazamwa kama kuongeza ushawishi wa Marekani barani humo baada ya Urusi na China kueneza ushawishi wake.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii