Watu 5000 waomba kazi jeshi la polisi Zanzibar

Watu zaidi ya 5000 wameomba nafasi ya kazi katika jeshi la polisi kamisheni ya Zanzibar, huku kamisheni hiyo ikihitaji kuajiri watu chini ya 500.


Kamishna wa Zanzibar, Khamis Hamad Khamsi amesema kati ya watu 5000 walioomba nafasi hizo, wenye sifa ni takribani watu  2,000, lakini wapo wenye sifa ambao  hawatachaguliwa kutokana na  naafsi kuwa chache.

Hayo yanajiri Baada ya jeshi la polisi kutangaza Nafasi za kazi  Desemba 5, 2022 na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Camillus Wambura kwa watu wenye sifa za stashahada, stashada ya juu, shahada na wahitimu wa kidato cha nne wenye ufaulu wa daraja la 1, 2, 3, 4 wenye alama 26, 27, 28 na 29.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii