Mwasa"Fuatilieni mafao yenu yanapelekwa wapi"

Mkuu wa Mkoa Kagera, Fatma Mwassa amewataka watumishi wa umma ndani ya Mkoa huo kutazama mafao yao kama yanapelekwa kwenye mfuko husika na kujua wameweka kiasi gani na kwamba jambo hilo liwe jukumu la watumishi wote wa Serikali kabla ya muda wao wa kustaafu.

Mwassa ametoa kauli hiyo wakati akihutubia watumishi katika sherehe za maadhimisho ya siku ya mei mosi kimkoa zilizofanyika katika viwanja vya Kaitaba vilivyopo manispaa ya Bukoba.

Amesema, “usipo fatilia mafao yako mapema kabla ya kustafu baadae itakuwa changamoto kubwa maana baadae miguu itakuwa haiwezi kutembea utakuwa unanyata na nauli haipo ya kutosha nawaomba mfanye hayo sasa watumishi wenzangu.”

Katika hatua nyingine, Mwassa, amesema Serikali itahakikisha inasimia mifuko yote ya jamii mkoani humo, itoe mafao ya wastaafu kwa wakati, ili yaweze kuwanufaisha wahusika

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii