Tanzania yatangaza masharti mapya ya Covid-19 kwa wasafiri wa kimataifa

Tanzania imetoa masharti mapya ya usafiri kwa wasafiri wanaoingia na kutoka nchini humo kama hatua ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya Covid -19.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Pro. Abel Makubi hatua hiyo inafuatia ongezeko la maambukizi mapya ya virusi vya corona.


Hatua hii inakuja saa kadhaa baada Umoja wa Falme za Kiarabu,UAE kutangaza kutasitisha safari za ndege kwa abiria kutoka Tanzania, Kenya, Ethiopia, na Nigeria na kuongeza vikwazo vya usafiri kwa ndege za Uganda na Ghana, kuanzia leo Jumamosi, Desemba 25.

Taratibu mpya zilizotowa na Wizara ya Afya ya Tanzania ni pamoja na:

  • Kuwa na cheti halali cha kipimo cha COVID-19 RT-PCR 
  • Kufanya kipimo cha haraka (COVID-19 Rapid Antigen Test) Uwanja wa Ndege ndani ya saa 6 kabla ya kusafiri kwa wasafiri wanaokwenda Marekani, India na baadhi ya nchi za Ulaya. 
  • Kufanya kipimo cha haraka cha PCR (COVID-19 Rapid PCR test) kama unaenda nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu, au kupitia Dubai. 
  • Wasafiri wote wanaunganisha usafiri wa ndege kupitia Tanzania wanapaswa kufanya kipimo cha haraka (COVID-19 Rapid Antigen Test) katika uwanja wa ndege ndani ya masaa 6 kabla ya kusafiri. 
  • Kuwa na cheti halali cha chanjo ya COVID-19

Hivi karibu Tanzania ilizindua mashine nyingine kubwa na ya kisasa kwa ajili ya kupima kipimo cha haraka cha Covid -19 kwa wasafiri wanaoenda nchi za Falme za Kiarabu, baada ya nchi hiyo kuwataka wasafiri wanaotokea Tanzania kwenda Dubai, kupata vipimo vya masaa 48 na kisha kumalizia na kipimo cha saa sita kabla ya safari.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii