Mtangazaji wa TV wa NBC Awa Gumzo

Mtangazaji wa TV Wa NBC ana trend baada ya kutumia Condom kufunika Mic yake akiwa na ripoti kuhusu Kimbunga Ian jimboni Florida. Kyla Galer aliwaambia watazamaji kuwa 'Hii ni condom, hatuwezi kulowesha hizi Mic'.

kimbunga hiki kimesababisha watu zaidi ya Milioni mbili kukosa umeme katika jimbo la Florida. 

Kimbunga hicho chenye nguvu, kinasababisha mafuriko makubwa katika barabara na makaazi ya watu huku upepo mkali ukishuhudiwa pamoja na mawimbi makali baharini. 


Kyla ni miongoni mwa waandishi wanaonyeshewa mvua usiku na mchana wakitoa ripoti ya kimbunga hicho.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii