Bunge la Israel lapiga kura ya kulivunja bunge na kufanya uchaguzi mpya

Bunge la Israel kwa kauli moja limeidhinisha muswada wa kulivunja bunge, hatua muhimu ya kisheria ambayo inaisukuma nchi hiyo kuelekea uchaguzi wake wa tano katika muda wa chini ya miaka minne. Tangu wiki iliyopita, wabunge wa muungano wa Waziri Mkuu anayemaliza muda wake Naftali Bennett na upinzani unaoongozwa na Waziri Mkuu wa zamani Benjamin Netanyahu wamekuwa wakizozana bungeni juu ya muswada wa kulivunjwa kwa bunge hilo la Knesset. Muungano huo ulisema ulitaka kuidhinishwa haraka kwa muswada huo baada ya Bennett kutangaza wiki iliyopita kwamba muungano wake wa vyama vinane uliogawika hauwezi tena kudumu. Hata hivyo Netanyahu na washirika wake wamekuwa wakifanya mazungumzo ya kutaka kuunda serikali mpya inayoongozwa na Netanyahu katika bunge la sasa, hatua ambayo ingeepusha kufanyika kwa uchaguzi mpya. Utayari wa upinzani kulivunja bunge unaonyesha kuwa juhudi za Netanyahu za kuunda serikali mpya zimekwama.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii