EACC Yataja Orodha ya Majina ya Viongozi Walioza Maadili, Wasiofaa Kuongoza Popote Kenya

Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) inaitaka Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuwazuia wagombea 241 kushiriki katika uchaguzi wa Agosti 9.
Mnamo Jumatano, Juni 1, tume hiyo ilitoa orodha ya wagombeaji wa kisiasa wanaokabiliwa na masuala ya uadilifu kwa hivyo hawafai kushikilia nyadhifa za serikali.
"Kufuatia uthibitishaji wa uadilifu wa wawaniaji 21,863 wa nyadhifa za uchaguzi, EACC imetambua 241 wenye masuala ya uadilifu na kuwasilisha ripoti hiyo kwa IEBC. EACC inawachukulia 241 hao kuwa wamekosa maadili na maadili ya uchaguzi hadi ofisi za umma," EACC ilisema.
Majina ya viongozi ni pamoja na:
Kiti cha urais

Wale ambao wameorodheshwa na wanaotafuta urais ni:
Wa Iria wa Usawa Kwa Wote Party, Justus Onyango wa Justice and Freedom Party na mgombea mwenza wa urais wa Chama cha Republican Matayo Jared.
Kiti cha useneta
Gavana wa Migori Okoth Obado anayewania kiti Migori kupitia People's Democratic Party, Danson Mungata mgombea wa UDA Tana River, Lillian Mbogo mgombeaji wa Jubilee Embu.
Kiti cha ugavana
Hao ni pamoja na Anne Waiguru anayegombea kupitia chama cha UDA, aliyekuwa gavana wa Nairobi Evans Kidero, Christopher Obure, Thuo Mathenge wa New Democrats anayewania kiti cha Nyeri, Jeremiah Loro Mukai mgombeaji wa Turkana wa ODM, Richard Leresian mgombea wa Jubilee Samburu, aliyekuwa waziri wa Petroli John Munyes anayegombea kupitia Jubilee Kaunti ya Turkana, Kofa Asman mgombea wa ANC wa kaunti ya Tana River na Gavana wa Tharaka Nithi Muthomi Njuki.
Kiti cha Ubunge

Oscar Sudi wa (Kapseret), John Waluke (Sirisia), Jonah Mburu (Lari), Samuel Arama ( Nakuru Mjini Magharibi), Fredrick Odhiambo (Ugunja), James Gakuya (Embakasi Kaskazini), Didmus Barasa (Kimilili), Alfred Keter (Milima ya Nandi) miongoni mwa wengine.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii