Uchaguzi Colombia kwenda duru ya pili Juni

Matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais nchini Colombia yanaonesha kutakuwa na duru ya pili mnamo mwezi Juni baada ya wagombea sita waliokuwa wakiwania kiti hicho kushindwa kupata asilimia 50 ya kura. Duru hiyo ya pili itamkutanisha mwanasiasa na mrengo wa kushoto Gustavo Petro aliyepata asilimia 41 ya kura dhidi ya Rodolfo Hernandez aliyejikingia asilimia 28 ya kura katika uchaguzi uliofanyika jana. Uchaguzi huo ulikuwa ni wa pili kufanyika nchini Colombia tangu serikali ya nchi hiyo ilipotia saini mkataba wa amani na waasi wa FARC mnamo 2016. Masuala makubwa yalikuwa ni kuongezeka kwa pengo la kipato kati ya watu matajiri na maskini pamoja na kupanda kwa bei za bidhaa. Gustavo anayejipigia upatu kuwa mwanasiasa asiyetokana na tabaka tawala ameahidi kuufanyia mageuzi uchumi wa Colombia ikiwemo suala la kodi pamoja na kukabiliana na magenge ya uhalifu wa silaha.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii