IEBC Yamwidhinisha Rasmi Johnson Sakaja Kuwania Ugavana wa Nairobi

Sasa ni rasmi kuwa Seneta wa Nairobi Johnson Sakaja atapeperusha bendera ya chama cha Uniited Democratic Alliance (UDA) katika kinyang'anyiro cha ugavana wa kaunti ya Nairobi katika uchaguzi wa Agosti 9.
Hii ni baada ya seneta huyo kufika mbele ya maafisa wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) na stakabadhi zake asubuhi ya Jumanne, Juni 7, na kupewa idhini ya kung'ang'ania kiti hicho.
Sakaja amekuwa na wakati mgumu wa kuwakabili wapinzani ambao wamekuwa wakieneza uvumi kuwa hajafuzu kimasomo.
Sakaja alisema kuwa washindani wake walikuwa wakiuza propaganda za kumchafulia jina na uadilifu wake kama kiongozi.
 Alihoji iwapo anafanana na mtu ambaye hajaenda shule, akieleza kuwa anazo stakabadhi za kuaminika na wala sio zile zilizokuwa zikitamba mtandaoni.
"Je, mimi nafanana na mtu ambaye hajaenda shule? Puuza propaganda zinazorushwa kote. Nina vyeti vingi vya masomo kuliko wanachokitafuta," alisema mbunge huyo.
Sakaja aanipa stakabadhi zake mtandaoni
Mnamo Ijumaa, Mei 27, mbunge huyo alianika stakabadhi zake za kitaaluma mtandaoni, na kuwakashifu wachochezi ambao walitilia shaka kuhusu kisomo chake.
Kilichoangaziwa zaidi na wapinzani wake mtihani wa shule ya upili ambao walisema alifeli.
"Tume ya Elimu ya Vyuo Vikuu (CUE) imeidhinisha na kutambua vyeti vyangu vya kitaaluma na hata kuishauri IEBC kuniidhinisha nigombee ugavana Agosti 2022, kaunti ya Kakamega. Wanaopenda propaganda wanaona aibu. Hizi hapa ni stakabadhi zangu halali," alisema.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii