Mgombea Huru Muthiora Kariara Achoma Kadi Yake ya Kura Kisa Kukataliwa na IEBC

Mwaniaji huru wa urais Muthiora Kariara aliamua kuchoma kadi yake ya kura kwenye ukumbi wa Bomas of Kenya, muda mchache baada ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kukosa kumuidhinisha.
Kariara alifika mbele ya tume hiyo siku ya Jumatatu, Juni 6, ila alikosa kupewa idhini ya kuwania urais kwa kutoweza kufikisha idadi ya saini za wafuasi zilizohitajika kuwania urais.
Hata hivyo, alipewa muda wa saa moja, kutafuta saini kutoka kwa kaunti tano.
Baada ya kukataliwa, mwaniaji huyo wa urais alinaswa kwenye video akichoma kura yake, mbele ya wanahabari pamoja na mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati.
Wakati wa kuchoma stakabadhi hiyo muhimu, Muthiora aliituhumu IEBC kwa kumuonea, hata baada ya kujitahidi kukusanya saini hizo kwa njia ya uaminifu.
"Inagharimu pesa nyingi kwa wale walioweza kupata stakabadhi hii. Kulikuwepo na watu waliokuwa wakichuuza vitambulisho vyao vya kitaifa kutoka jumba la Harambee, walakini tulichukua njia ya kweli ila haitatufaa," Muthiora alilalama.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii