Mwanamuziki Kevin Bahati anaonekana kuwa vitani kwa wiki kadhaa sasa na mkewe Diana B kuhusu chaguo lake la mavazi hususan baada ya kuzindua taaluma yake ya kisiasa.
Msanii huyo ambaye analenga ubunge wa Mathare kwa tiketi ya chama cha Jubilee, alisema Bahati Sasa Amfokea Mkewe Diana B Kuhusu Mavazi: "Anza Kuvalia Kama Mke wa Mheshimiwa" Read more:
Bahati ambaye anatambulika na vibao kadhaa kama vile Barua, Machozi na Itakuwa Sawa anahoji kuwa nidhamu ya mavazi ni kwa ajili ya wapiga kura wa Mathare kwa sasa Diana ni mke wa Mheshimiwa.
"Unafaa kuheshimu wapiga kura wangu. Mbona unavaa nguo zilizoraruka? Unafaa kujua wewe ni mke wa Mheshimiwa. Unafaa kujua kuwa watu wanakuangalia,” Bahati alisema
Hata hivyo kwa upande wake, Diana ambaye pia ni msanii japo wa kuchana, alisema kuwa wapiga kura hawakuangazia kaptura yake iliyochanikwa aliyokuwa amevalia kwenye ziara yao ya kampeni mtaani Mathare.
“Tulipokwenda Mathare kupeana unga, nilienda hivi na hakuna aliyelalamika,” Diana B alijitetea.