Rais wa Tunisia ashutumiwa kwa kudumaza taasisi za kidemokrasia

Rais wa Tunisia, Kais Saied kwa kudumaza taasisi za kidemokrasia za nchi hiyo baada ya kuwafukuza kazi majaji kadhaa huku kukiwa na safu ya hatua ambazo zilionekana kulenga kuunganisha utawala wa mtu mmoja.

Rais Saied ambaye pia amefanya mabadiliko kwenye nafasi ya tume huru ya uchaguzi na kusema kwamba atazindua katiba mpya mwezi huu aliwashutumu majaji hao kwa rushwa na kuwalinda magaidi katika hotuba yake kwa njia ya televisheni siku ya Jumatano.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Marekani, Ned Price alisema uondoaji huo ni sehemu ya mwenendo wa kutisha wa hatua ambazo zimedhoofisha taasisi huru za kidemokrasia nchini Tunisia.

Maafisa wa Marekani waliwasiliana na wenzao wa Tunisia kutathmini umuhimu wa kuangalia na kuleta uwiano katika mfumo wa kidemokrasia Price alisema wakati wa mkutano wake wa kawaida na waandishi wa habari.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii