Kinachofanyika katika mwili wako unapofunga hadi saa 20 katika siku 30

Kila mwaka, mamilioni ya Waislamu hufunga wakati wa kutoka kwa jua hadi machweo kwa siku 30 kama sehemu ya likizo ya Ramadhani.

Katika miaka ya hivi karibuni, Ramadhani imekuwa ikisherehekewa sanjari na miezi ya kiangazi katika ulimwengu wa kaskazini, wakati siku ni ndefu na joto kali.

Ukweli ni kwamba mwili hauingii moja kwa moja katika mazoea ya kufunga hadi saa nane ya chakula chako cha mwisho. Hili hutokea wakati mfumo wa kusaga chakula mwilini unapomaliza kupokea virutubisho kutoka kwa chakula.

Muda mfupi baadaye mwili hutumia sukari iliyopo katika maini na mkisuli ili kutoa nguvu mwilini. Wakati glucose inapoisha mwilini chanzo chengine cha kupata nguvu mwilini huwa mafuta.

Wakati mwili unapoanza kuchoma mafuta hayo , husaidia kupunguza uzani , hupunguza kiwango cha mafuta mwilini na kupunguza hatariu ya kupata kisukari. Hatahivyo kupungua kwa viwango vya sukari katika damu husababisha mtu kuhisi udhoofu . Wakati huo mtu uhisi kichwa kuuma na kisunzi.

Ni wakati mtu anahisi njaa zaidi

Jichunge na ukosefu wa maji mwilini: Siku ya 3 hadi ya 7

Huku mwili wako ukiendelea kuzoea kufunga , mafuta hubadilishwa na kuwa sukari ndani ya damu . Unapokosa kunywa maji wakati wa kufunga , basi nyakati za usiku hutumika kujaliza maji yaliokosekana mwilini, la sivyo mtu anapotokwa na jasho usiku anaweza kupatikakan na tatizo la ukosefu wa maji mwilini.

Vyakula vyote vinapaswa kuwa na viwango vya juu vya vyakula vinavyokupa nguvu kama vile carbohydrates na mafuta. Ni muhimu kuwa na chakula chenye virutubisho kama vile, Protini, chumvi na maji.

Mwili unaanza kuzoea kufunga: Siku ya 8 hadi 15

Katika awamu ya tatu , utaona hali ya wanaofunga ikiimarika huku miili yao ikizoea kufunga.

Dkt. Razeen Mahroof, mshauri katoka sindano za kulemaza na matibabu muhimu katika chuo cha matibabu cha Addenbrook cmbridge anasema kwamba kuna manufaa mengine.

"Katika maisha ya kawaida ya kila siku, mara nyingi tunakula kalori nyingi, na hii inaweza kuzuia mwili kufanya kazi zingine vizuri, kama vile kujirekebisha."

"Hii inasahihishwa wakati wa kufunga kwa sababu inaruhusu mwili kuelekeza umakini kwa kazi zingine.

Kwa hivyo kufunga kunaweza kunufaisha mwili kwa kuwezesha uponyaji na pia kuzuia na kupambana na maambukizo."

Wakati wa kipindi cha katikati cha Ramadhani, mwili huwa umezoea mchakato wote wa kufunga .

Tumbo, ini, figo na ngozi zitapitia kipindi cha kuondoa sumu katika hatua hii.

"Kiafya, katika awamu hii, kazi ya viungo mbalimbali inapaswa kurudi kwa uwezo kamili. Ubongo wako unapaswa kuimarika na unaweza kuwa na nguvu zaidi," anasema daktari.


"Mwili haugeukii protini kwa ajili ya kupata nguvu. Huu ndio wakati unapoingia kwenye hali ya 'njaa' na kutumia misuli kupata nguvu hizo. Hali hii hutokea kwa kufunga kwa muda mrefu mfululizo kwa siku nyingi hadi wiki."

"Kwa kuwa mfungo wa Ramadhani hufanyika tu kuanzia alfajiri hadi jioni, kuna fursa nyingi za kujiboresa kwa vyakula na maji ya kuupatia mwili nguvu. Hatua hii uhifadhi misuli lakini pia husaidia kupunguza uzito."

Hivyobasi tunauliza je kufunga ni muhimu kunsaidai afya yako?

Dkt Mahroof anasema ndio lakini kwa masharti.

"Kufunga ni kuzuri kwa afya zetu kwa sababu hutusaidia kuzingatia kile tunachokula na wakati gani. Hata hivyo, ingawa kipindi cha kufunga kwa mwezi kinaweza kuwa kizuri, haipendekezi kufanya hivyo kwa kuendelea."

"Mfungo wa kuendelea sio mzuri kwa sababu unaweza kupoteza uzani wako kwa muda mrefu na hatimaye mwili kuacha kubadilisha mafuta ili kupata nguvu, na badala yake kuyageuza kuwa misuli. Hii ni hatua mbaya na husababisha mwili kudhoofika.

Daktari huyo anapendekeza kwamba mbali na ramdhan, kufunga kwa siku kadhaa wakati wa siku za kawaida , huenda kukasaidia afya yako badala ya kunedelea kufunga kwa miezi mingi.

''Kufunga wakati wa mwezi wa ramadan , iwapo kutafanywa kwa usahihi, kunapaswa kukusaidia kuimarisha usambazaji wa nguvu mwilini kila siku , hatua ambayo humaanisha mtu anapunguza uzani wake bila ya mwili kuchoma tishu muhimu za misuli''

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii