Je, Rwanda ni nchi ya usalama au hofu?

Wageni wanaotembelea Rwanda mara nyingi huvutiwa kupata nchi ambayo mambo yanaonekana kufanya kazi kwa ufanisi. Ni nadhifu na mwonekano wa kijani kibichi - na huduma ya wi-fi ni nzuri katika mji mkuu, Kigali.

Kila mtu huwa na tabia ya kulipa kodi; huduma ni za kuaminika; barabara ni salama - serikali inaita "moja ya mataifa salama zaidi duniani".

Chukua janga la Covid kwa mfano. Rwanda haikusita kupambana na Covid moja kwa moja na kutekeleza vikwazo haraka na kwa njia madhubuti. Leo zaidi ya 60% ya watu wamechanjwa - jambo ambalo Jarida la Matibabu la Uingereza linaita mafanikio "katika bara ambalo ni jangwa la chanjo ya Covid-19".

Lakini chini ya hilo na mapambo ya maua jijini Kigali ni hofu ya pamoja.

Tembea kwenye baa na ujaribu kuanzisha mjadala wenye utata, na utafungwa - na kuna uwezekano mkubwa kwamba tabia yako itaripotiwa kwa mamlaka.

Wale wanaoonekana kuwa tishio la kweli watachukuliwa hatua kali.
"Inaonekana kama Uswizi ya Afrika lakini ni nchi ya ukandamizaji na ya kutisha," Michela Wrong, mwandishi wa kitabu cha hivi punde kuhusu Rwanda kiitwacho 'Do Not Disturb'.
Katika Jumamosi ya mwisho ya kila mwezi, kila mtu hukusanyika katika vitongoji vyao kufanya usafishaji wa pamoja - barabara zinafagiliwa, takataka zinakusanywa. Inaitwa Umuganda, ambayo kwa Kinyarwanda inamaanisha "Kazi ya Kijamii".
Mnyarwanda mmoja, ambaye aliomba jina lake lisitajwe, anaeleza hakuna sheria inayolazimisha watu kuhudhuria Umuganda - lakini kuna hofu kwamba utapata sifa mbaya , mtu atakuripoti, kwamba jina lako litaandikwa kuwa mkorofi.
Kambi yoyote ambayo wanaotafuta hifadhi wanatumwa chini ya mkataba mpya wa Uingereza inaweza kuwa jambo lililopangwa vyema - sio kambi za wakimbizi ambazo wakati mwingine unaona mahema au karatasi za plastiki .
Nchi hiyo, ambayo ina wakazi milioni 13, tayari imechukua zaidi ya Waafrika wanaotafuta hifadhi kutoka Libya 900 tangu 2019 - chini ya makubaliano na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) na Umoja wa Afrika (AU).
Eneo la Gashora linalosimamiwa na Umoja wa Mataifa lina miundo ya kudumu - na wengi wa wale ambao wametoka Libya wameendelea na maisha yao
Wamewekwa katika eneo la Gashora, takriban kilomita 60 kutoka Kigali. UNHCR inasema sio kambi ya wakimbizi, bali ni Mfumo wa Dharura wa Usafiri - na zaidi ya nusu yao tayari wamehamishiwa Sweden, Canada, Norway, Ufaransa na Ubelgiji.
Eneo hilo la Umoja wa Mataifa, ambalo lina miundo ya kudumu, inalenga kuwafundisha wale waliokabiliwa na hali mbaya katika kambi za Libya, ujuzi wa kuwasaidia katika maisha yao mapya. Kambi hiyo ina shule ya udereva na inatoa mafunzo ya lugha, miongoni mwa mambo mengine.
Lakini Denmark ilipotangaza mwaka jana kuwa inapanga mpango sawa na ule ambao Uingereza imezindua hivi punde, AU iligoma.
"Jaribio kama hilo la kukomesha uhamaji kutoka Afrika kwenda Ulaya ni chuki dhidi ya wageni na halikubaliki kabisa," ilisema Agosti mwaka jana.
Afrika tayari imebeba asilimia 85 ya wakimbizi duniani "mara nyingi katika hali ya muda mrefu, ambapo ni asilimia 15 tu ndio wanaohifadhiwa na nchi zilizoendelea", ilisema.


"Yote ni kuhusu kutuma kizuizi kwa wanaotafuta hifadhi... mtu yeyote ambaye anajaribu kukimbia ukandamizaji barani Afrika ataogopa kutumwa Rwanda," alisema.
Tofauti na mradi wa UNHCR, maelezo yanayotolewa kuhusu mpango wa Uingereza yanapendekeza kwamba wanaotafuta hifadhi watakuwa nchini Rwanda kwa muda mrefu - "ili waweze kuishi na kustawi", kama waziri wa mambo ya ndani alivyosema.
Haijabainika ni watu wangapi Rwanda inatarajia kukubali, ikizingatiwa kuwa ni moja ya nchi zenye watu wengi zaidi barani Afrika lakini Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson alisema itachukua "makumi ya maelfu katika miaka ijayo".
Nje ya Kigali, Wrong anasema ni "jamii maskini ya kilimo ambapo kila inchi ya ardhi yenye rutuba inalimwa na ambayo haina nafasi ya kuchukua wakimbizi".
Hakuna anayetarajia upinzani mkubwa nyumbani kwa hatua hiyo - kwani wakosoaji wa Paul Kagame mwenye umri wa miaka 64, ambaye aliongoza vikosi vya waasi vilivyomaliza mauaji ya kimbari ya 1994 na amekuwa rais tangu 2000, wanaelekea kujutia.
Mwezi uliopita, Human Rights Watch ilitoa ripoti kuhusu mashtaka katika mwaka jana ya angalau wanaYouTube wanane wanaochukuliwa kuwa wakosoaji wa serikali. Mmoja, ambaye alipiga picha na kukosoa askari wanaowafukuza wakazi kwa nguvu wakati kuondoa nyumba za makazi duni, amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela.
Wakosoaji wanaoikimbia nchi hiyo wamekuwa wakifuatiliwa na kuuawa na maajenti wa Rwanda waliokuwa uhamishoni - au katika kesi ya Paul Rusesabagina, meneja wa hoteli ambaye aliokoa maisha ya zaidi ya watu 1,000 wakati wa mauaji ya kimbari na ambayo filamu ya Hollywood Hotel Rwanda ilitungwa alifunguliwa kesi.
Paul Rusesabagina, ambaye aliigizwa na Don Cheadle katika filamu ya Hollywood Hotel Rwanda, anatumikia kifungo cha miaka 25 jela.
Baada ya mauaji ya kimbari - ambapo watu 800,000 waliuawa - Rusesabagina alikuwa raia wa Ubelgiji na alitumia umaarufu wake kupaza sauti dhidi ya kile alichosema kuwa utawala kandamizi wa Rais Kagame.
Lakini mwaka 2020, familia yake inasema alitekwa nyara alipokuwa akipitia Dubai na kupelekwa Rwanda na amehukumiwa kifungo cha miaka 25 jela kwa kuunga mkono kundi la waasi.
Binti yake, Carine Kanimba, aliiambia BBC kuwa ilionyesha Rwanda haiheshimu haki za binadamu: "Rwanda ni udikteta, hakuna uhuru wa kusema, hakuna demokrasia. Katika uchaguzi uliopita rais alishinda uchaguzi kwa 99% ambayo inakuambia hii sio demokrasia.
"Sielewi kwa nini serikali ya Uingereza ingeamua kupeleka watu wasiojiweza katika nchi ambayo inajulikana kuwakandamiza watu wake."
Sababu labda iko kwenye mlango wa Bw Kagame, ambaye ana urefu wa zaidi ya futi 6, ni mtu mwenye mvuto, anayependa klabu ya soka ya Arsenal na mwenye msukumo . Viongozi wengi wa Magharibi - wale ambao wanaweza kuhisi hatia ya kutofanya zaidi kukomesha mauaji ya kimbari ambayo yanaitambua Rwanda kwa watu wengi wa nje - wanavutiwa naye.
President Paul Kagame visits the Gahanga Cricket Oval, during the official inauguration, on 28 October 2017
"Yeye ni mzuri sana katika kutambua masuala ambayo yanawafanya viongozi wa nchi za Magharibi kukosa usingizi na kuyapatia ufumbuzi ambao unaonekana kuwa na ufanisi na wa bei nafuu," anasema Wrong, akionyesha jinsi wanajeshi wa Rwanda walivyotumwa Msumbiji mwaka jana kushughulikia uasi wa kijihadi.
Mwaka jana, Bw Kagame alisema alikuwa akitoa vituo vya wakimbizi kwa "misingi ya kibinadamu". Moja ya vyama vichache vya upinzani nchini Rwanda vimesema yote ni kwa sababu ya pesa.
Mataifa ya Magharibi yamefurahishwa na maendeleo ya haraka ya kiuchumi ya Rwanda tangu mauaji ya halaiki na kwa ukweli kwamba rushwa inaonekana si suala - ingawa wafadhili wanatoa ilani kuhusu haki za binadamu.
Mapenzi ya chama cha Conservative cha Uingereza na Rwanda yalianza mwaka 2007, wakati upinzani, na kitu kiitwacho Project Umubano, kilichoanzishwa na Andrew Mitchell.
Waziri wa zamani wa maendeleo alipanga wabunge kusafiri nje kila mwezi Agosti kufanya kazi katika miradi ya maendeleo - na kufundisha kriketi.
Shirika la misaada la kriketi lililohusishwa na mradi huo lilianza kuchangisha fedha na miaka michache iliyopita uwanja wa kisasa wa kriketi wa Gahanga, unaojulikana pia kama Kicukiro Oval, ulifunguliwa nje kidogo ya Kigali.
Baadhi wanaona mpango wa kutafuta hifadhi kama sehemu ya mkakati wa hali ya juu wa kuboresha taswira ya Rwanda, wakati nchi hiyo inapojiandaa kuandaa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Madola mwezi huu wa Juni.
Lakini msemaji wa serikali ya Rwanda aliwapuuza wakosoaji wake, akisema hakuna mtu aliyeteswa nchini Rwanda kwa kuwa na maoni yake.
"Tunajua aina ya hali ambazo watu kutoka nchi kama hizo wamepitia na hapa ni mahali ambapo watakuwa salama, watalindwa na wanaweza kuishi maisha ya heshima na kupata fursa ya kukuza vipaji vyao," Yolande Makolo aliwaambia waandishi wa habari.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii