COP31 Yaaanza kwa mvutano wa fedha za tabianchi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amewataka viongozi wa dunia kuchukua hatua za haraka na za dhati dhidi ya mabadiliko ya tabianchi wakati mkutano wa COP31 ukianza jijini Antalya, Uturuki.

Akizungumza muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano huo wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa kuhusu tabianchi, Guterres amesema dunia haiwezi kuendelea kuchelewesha hatua wakati athari za mabadiliko ya tabianchi zikizidi kuongezeka na kuathiri maisha ya watu pamoja na uchumi wa mataifa mbalimbali.

Mkutano huo unafanyika baada ya mwaka ulioshuhudia mawimbi makali ya joto barani Ulaya, moto mkubwa wa misitu nchini Indonesia na mafuriko mabaya nchini Nepal, huku hali ya hewa ya El NiƱo yenye nguvu isiyo ya kawaida ikichangia kuongezeka kwa matukio ya hali mbaya ya hewa duniani.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii