Navi Pillay, aliyekuwa Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu kwenye Umoja wa Mataifa, kati ya mwaka 2008 hadi 2014, ndio mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel kwa mwaka 2026.
Jørgen Watne Frydnes, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Nobel, wakati akimtangaza Pillay kama mshindi, amesema amepata tuzo hiyo kutambua kazi yake ya kuhimiza amani na sheria ya kimataifa.
Navi Pillay, akizugumza akiwa nchini Ujerumani, amesema tuzo hii inaitoa kwa waathiriwa wote wa ukiukwaji wa haki za binadamu.
Mzaliwa huyo wa Afrika Kusini, alishika wadhifa wa Mkuu wa Tume ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kati ya mwaka 2008 hadi 2014.
Navi Pillay mwenye umri wa miaka 85, aliwahi pia kuwa Jaji katika Mahakama ya Kimataifa kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda, na alikuwa mstari wa mbele kupinga matumizi ya nguvu wakati wa maandamano katika nchi za Libya na Syria.
Kwa sasa ni Jaji, katika Mahakama ya Haki, akisikiliza kesi kuhusu madai ya kimbari nchini Gambia na Mynamar.
Aidha, ni rais wa Tume ya Kimataifa dhidi ya mauaji adhabu ya kifo yenye makao yake jijini Madrid.
Mwaka 1995, baada ya kukamilika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi, Pillay alihudumu kama Jaji katika Mahakama ya Kuu nchini Afrika Kusini.
Mwaka 2003, aliwahi pia kuhudumu kama Jaji, katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC yenye makao yake jijini Hague, hadi mwaka 2008.
Anashikilia rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza, kuanzisha kampuni yake ya sheria, katika mkoa alikozaliwa wa Natal mwaka 1967, akipigania haki za wafungwa katika kisiwa cha Robben.