Ndege zisizo na rubani za Ethiopia zimeshambulia mara kwa mara wanajeshi wa Eritrea waliotumwa hivi karibuni kuzunguka mji wa Adigrat kaskazini mwa mkoa wa Tigray wa Ethiopia, ambao unapakana na Eritrea, tangu Jumatano jioni, mashahidi na shirika lisilo la kiserikali la ACLED.
Hali inazidi kuwa mbaya kati ya majirani hao wawili wa Pembe ya Afrika, na kuzua hofu ya vita mpya baada ya ile iliyowakutanisha kati ya mwaka 1998 na 2000.
Kulingana na ACLED, shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na uchambuzi wa migogoro ya kivita duniani kote, mashambulizi "mengi" ya ndege zisizo na rubani yalilenga "wanajeshi wa Eritrea na vifaa vya kijeshi na risasi vilivyopakiwa kwenye magari ya kijeshi" karibu na Adigrat kuanzia siku ya Jumatano jioni hadi Alhamisi asubuhi.
Kulingana na wakazi wa Adigrat, vikosi vya Eritrea vilivyokuwa vimetumwa katika siku za hivi karibuni katika mji huu, ulioko takriban kilomita 40 kusini mwa mpaka wa Eritrea, na pia kusini zaidi kuelekea mji mkuu wa kikanda wa Mekele, vimeonekana vikijiondoa kaskazini mwa mji.
Hali inazidi kuwa mbaya kati ya majirani hao wawili wa Pembe ya Afrika, na kuzua hofu ya vita mpya baada ya ile iliyowakutanisha kati ya mwaka 1998 na 2000.
Mkazi wa Adigrat, akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, "mashambulizi mengi ya ndege zisizo na rubani" usiku wa kuamkia leo Alhamisi, akiongeza kwamba "malori ya Eritrea yaliharibiwa." Ameongeza, "Askari wa Eritrea hawapo tena mitaani mwa Adigrat; uvumi ni kwamba wamekimbilia vilimani" kaskazini mwa jiji.
Walipoulizwa kuhusu hali ya mambo kaskazini mwa Ethiopia, mamlaka za Asmara wala zile za Addis Ababa hazijatoa majibu yoyote kwa sasa.
Vikosi vya Eritrea viliunga mkono jeshi la shirikisho la Ethiopia wakati wa vita vya awali vya Tigray, vilivyoendelea kati ya mwaka 2020 na 2022 kati ya Ethiopia na kundi la Tigray People's Liberation Front (TPLF), kundi la kisiasa lililoitawala Tigray na kukaidi mamlaka ya shirikisho.
Makubaliano ya amani yaliyosainiwa mwaka wa 2022 yaliplekea kusitishwa kwa vita, lakini hayakuzuia kuanza tena kwa mivutano na uhasama mnamo Septemba 23 kati ya serikali ya shirikisho ya Ethiopia na TPLF, ambayo Addis Ababa sasa inaishutumu Asmara kwa kuiunga mkono.