Watumiaji dawa za kulevya hatarini kuugua saratani ya kinywa

WATUMIAJI wa dawa za kulewamo hatarini zaidi ya maradhi ya kinywa, huku uharibifu wa meno ukiwa Kwa kiwango kikubwa, ukilinganisha na watu wengine.

Miongoni mwa dawa hizo zinazoleta athari kwenye afya ya kinywa na meno, ni bangi, methamphetamine, cocaine na heroin.

Bingwa bobezi katika afya ya kinywa na meno, Dk. Baraka Nzobo, amesema hayo akizungumza na gazeti hili, kuhusu kundi hilo la watumiaji dawa hizo na athari zake kwa ujumla.

Amesema kwamba matumizi ya dawa za kulevya husababisha uharibifu mkubwa wa meno na fizi, yakiwamo meno kuoza, fizi kuvimba, kuoza na meno kung'oka yenyewe hivyo kumfanya mtu kuwa na mapengo ama kibogoyo.

"Baadhi ya dawa za kulevya na madhara kwenye kinywa cha mtumiaji. Methamphetamine, matumizi ya dawa hii ya kulevya husababisha madhara ya fuatayo kwenye kinywa cha mtumiaji, kuwa na kinywa kikavu (xerostomia).

"Mate hupungua, hivyo meno hukosa ulinzi wa asili wa kuzuiwa kutoboka/kuoza. Kuoza kwa meno ni kwa kasi kubwa sana (Meth Mouth), hasa kwenye sehemu za shingo ya jino," amesema Dk. Nzobo, ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi idara ya Kinywa na Meno, Wizara ya Afya.

Ameongeza kuwa pia baadhi ya watumiaji WA dawa hiyo husaga meno yao bila kujitambua wakiwa chini ya ushawishi wa dawa na hivyo kuyavunja au kuyachakaza.

"Humsababishia mtumiaji kupata tamaa ya kupata vinywaji/vyakula vyenye sukari nyingi ambavyo husababisha kwa kiasi kikubwa meno kuoza."

Kwa upande wa cocaine, ameeleza kwamba ikitumika kwa kupaka kwenye fizi huharibu tishu za fizi moja kwa moja, wakati mwingine kusababisha vidonda kwenye fizi, hasa fizi kutoa usaha au kuiozesha fizi.

Pia amesema cocaine inaongeza hatari ya ugonjwa wa mbaya wa fizi unaoshambulia mfupa unaoshikilia jino hali inayofanya meno kulegea na hatimaye kung’ooka yenyewe na hivyo kumfanya mtumiaji kuwa na mapengo.

"Husababisha gamba gumu la jino kumomonyoka wa meno kutokana na tindikali inayopatika kwenye cocaine."

Kuhusu bangi, bingwa huyo amesema mvuta bangi hukumbana na athari zifuatazo kwenye Kinywa chake kinywa kukauka, hali inayomsababishia kuongea sauti ya mikwaruzo lakini pia kutobokaau kuoza kwa meno.

"Kuna ongezeko la hatari ya kupata saratani ya kinywa. Humfanya mtumiaji kuwa na uzembe wa kufanya usafi wa kinywa kutokana na athari za kiakili azipatazo kwa ajili ya bangi."

Pia amesema watumiaji wa heroin, hupata madhara kwenye kinywa chake, ikiwamo tamaa kubwa ya kula au kunywa vitu vyenye sukari nyingi, hali ambayo huongeza hatari ya kuoza kwa meno.

"Humfanya mtumiaji kupuuza usafi wa kinywa kutokana na athari za kiakili azipatazo mtumiaji wa heroin.

Kinywa kukauka, hivyo kufanya meno kukosa ulinzi wa asili wa mate na kuyafanya kuoza au kutoboka kwa urahisi.

"Sababu za ziada zinazochangia madhara ya dawa za kulevya kwenye afya ya kinywa, ni mtumiaji dawa za kulevya huwa na hali ya lishe duni na wakati mwingine kutokula vizuri.

"Mtumiaji dawa za kulevya huwa na hali ya Kutozingatia usafi wa kinywa (kutopiga kupiga mswaki meno yake inavyotakiwa au kutopiga kabisa mswaki)," amefafanua.

Dk. Nzobo ameongeza kwamba, mtumiaji dawa za kulevya kutopata huduma za afya ya kinywa mara kwa mara kutokana na kuathirika na dawa za kulevya, kunasababusha kuchelewa kwenda hospitali kupata huduma za matibabu mpaka hali ya kinywa chake inavyokuwa mbaya.

"Tabia ya kutumia sukari nyingi, hamu ya vitu vitamu inayosababishwa na baadhi ya dawa, ni hatari kiafya," amesema.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii